MAPISHI - Wali Wa Samaki Na Mboga
VIPIMO VYA SAMAKI
Samaki wa sea bass vipande 1 1/2 LB (Ratili)
Thomu iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga 1 kijiko cha chai
Chumvi Kiasi
Ndimu
Mafuta 3 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.
2. Washa oven moto wa 400F.
3. Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
4. Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.
VIPIMO VYA MBOGA
Gwaru (green beans) 1 LB
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Karoti 4-5
Chumvi Kiasi
Bizari ya manjano 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
2. Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru, halafu weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
3. Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
4. Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.