MAPISHI - Wali Wa Kichina Na Mayai
Vipimo
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Mbogamboga za barafu
(karot, njegere, spring beans na mahindi) 1 kikombe
Kuku Kidari 1 LB (ratili)
Mayai 2 mayai
Vitunguu (vikubwa) 2 au 3 vidogo
Pili pili manga 1 kijiko cha chai
Paprika 1 kijiko cha chai
Chumvi Kiasi
Mafuta 1/3 kikombe cha chai
Thomu 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu 1
Soy sauce 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
1. Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.
2. Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina) kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.
3. Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.
Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali
1. Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
2. Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi, uache uchemke hadi ukaribie kuwiva. Chuja maji.
3. Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu, kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka. (crumbled egg)
4. changanya mchanganyiko wa kuku na mboga. Kisha tia wali changanye vizuri.
5. Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive.
6. Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.