MAPISHI - Wali Maharage Na Kamba Wa Rojo
Vipimo:
Wali:
Mchele 2 Vikombe
Maji 3 1/2 Vikombe
Chumvi kiasi
Maharage:
*Maharage 4 Vikombe
Kitunguu 1 kidogo
Nyanya 1
Pilipili mbichi au ya mbuzi (ukipenda) 2 au 3
Tui la nazi zito 2 Vikombe
* Ikiwa maharage makavu, osha na roweka kwa muda wa masaa, kisha uchemshe yaive. Au tumia ya tayari ya kopo.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali
Kama kawaida ya kupika wali mweupe;
1. Osha mchele, roweka.
2. Chemsha maji umimine mchele, tia chumvi.
3. Funika uive moto mdogo mdogo.
4. Ukipenda wali wa kuchuja maji, ongeza kiasi cha maji.
Namna ya Kutayarisha na Kupika Maharage:
1. Tia maharage katika sufuria, uweke kwenye moto.
2. Tia tui zito.
3. Katia katika vitunguu, nyanya, pilipili, tia na chumvi.
4. Acha yapikike hadi upendavyo kiasi cha tui kubakia katika maharage.
5. Epua na tayari kuliwa na wali au aina yoyote ya mikate.
Kamba:
Fuata maelezo ya utayarishaji na upikaji katika mapishi yafuatayo:
Kamba Wa Rojo