MAPISHI - Pilau Ya Tuna Na Mboga
Vipimo
Mchele 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen veg)
Tuna 2 kopo
Thom na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 2
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 2 vijiti
Karafuu 6 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Viazi 3
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
2. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
3. Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
4. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
5. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
6. Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
7. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.