MAPISHI - Pilau Ya Sosi Ya Soya Na Mboga

sss


 
 VIPIMO


Kuku (mkate mkate vipande)                                       1

Mchele wa Basmati (rowanisha)                                  3 magi

Mdalasini                                                                       1 mchi mmoja                      

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba)                 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu                            1 magi

(karoti, mahindi, njegere)

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba)                     1 magi

Pilipili mbichi (iliyosagwa)                                             3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo             1

Pilipili manga                                                                 1 kijiko cha chakula

Chumvi                                                                          1 kijiko cha chakula

Sosi ya soya (soy sauce)                                              5 vijiko vya chakula

Kotmiri iliyokatwa katwa                                             1  magi

Thomu na tangawizi iliyosagwa                                   2 vijiko vya chakula

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.  Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.

2.  Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku awive na maji yakauke.

3.  Changanya vitunguu  ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .

4.  Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja. Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.

5.  Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.

6.  Weka moto mdogo mpaka wali ukishawiva.  Uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO:

Unaweza kuupika wali huo ndani ya jiko, yaani badala ya kutia masala kwenye sufuria ukayatia katika bakuli au treya ya jiko (oven), kisha ukamwagia wali uliouchuja humo na kuupika kaitka moto wa 400-450 Deg kwa muda wa dakika 15-20.









MAPISHI :  Je unapenda kupika lakini hujui? kama jibu ndio basi karibu sana katika page hii ya mapishi ambayo utapata machache ambayo yatakusaidia katika masuala mazima kuhusu kupika.

Powered by Pnyxe








Free Web Hosting