MAPISHI - Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya
Vipimo
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Nyama ya ngo’mbe 1 kg
Pilipili boga 1 kubwa
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Ndimu 1
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Mdalasini ½ kijiko cha chai
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na Kupika
1. Roweka mchele wako katika chombo
2. Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi
3. Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi
4. katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni
5. Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia
6. Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto
7. Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya
8. Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi
9. Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke
10. Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza
11. Funika na punguza moto na uache uive taratibu
12. Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.