MAPISHI - Pilau Ya Kuku
Vipimo
Mchele wa basmati 3 vikombe
Kuku ½
Viazi 4
Vitunguu 2
Thomu iliyosagwa 2 vijiko vya supu
Binzari ya pilau nzima 1 Kijiko cha chakula
Binzari ya pilau ½ kijiko cha chai
Pilipili manga nzima ½ kijiko cha chai
Karafuu nzima 8
Iliki nzima 6
Mdalasini nzima 5 vijiti
Pilipili mbichi iliyosagwa 2
Chumvi kiasi
Mafuta ya kupikia ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
3. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
4. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
5. Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
6. Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
7. mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.