MAPISHI - Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga
Vipimo
Mchele 2 Mugs
Viazi 3
Nyama ya Kusaga 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen vegetable)
Thom na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 1
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 1 vijiti
Karafuu 3 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele.
2. Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando.
3. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
4. Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive.
5. Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu.
6. Tia mboga ya barafu (frozen vegetables)
7. Tia maji, kidonge cha supu.
8. Yatakapochemka tia mchele.
9. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.