MAPISHI - Biskuti za kastad
VIPIMO
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe
laini (creamy).
2. Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
3. Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
4. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
5. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
6. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.