MAPISHI - Biskuti za kastad
VIPIMO
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi ½ kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
2. Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.
3. Tia unga na baking powder na Kastadi.
4. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray).
5. Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.