MAPISHI - Biskuti za jam
VIPIMO
Unga 2 ½ gilasi
Sukari ¾ gilasi
Samli 1 gilasi
Mayai 2
Baking powder 2 kijiko vya chai
Vanilla 1 ½ kijiko cha chai
Maganda ya chungwa 1
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.
2. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.
3. Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.
4. Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.
5. Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.
6. Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.
7. Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula..