MAPISHI - Biskuti za chumvi
VIPIMO
Unga 3 Vikombe vya chai
Siagi 250 gms
Baking powder 3 Vijiko vya chai
Mayai 2
Chumvi 1 kijiko cha chai
Maziwa 1/2 Kikombe
Pilipili manga ya unga 1 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream).
2. Tia Unga, baking powder, pilipili manga.
3. Tia maziwa.
4. Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda.
5. Pika (bake) katika moto wa 350º C – usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.