MAPISHI - Biriyani Ya Kuku (kavu)
VIPIMO
Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu
Kuku (Mkate kate Vipande) 4 LB
Thomu na Tangawizi paste 2 tablespoon
Chumvi kiasi
Pilipili nyekundu ya unga 1 tablespoon
Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) 1 teaspoon
Bizari ya pilau ya powder (Jeera) 1 teaspoon
Gilgilani powder (Dania) 1 teaspoon
Ndimu 1 tablespoon
Mchele na vitu vya Masala:
Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) 7 cups
Mafuta ya kupikia kiasi
Vitunguu 8 Medium
Tomatoes (chopped) 3 medium
Thomu na Tangawizi paste 1 tablespoon
Garam Masala 1 tablespoon
Hiliki powder ½ teaspoon
Tomatoe paste 1 tablespoon
Pilipili mbichi zipasue katikati 4
Chumvi kiasi
Mtindi 4 tablespoon
Kotmiri iliokatwa (Chopped) ½ cup
Mafuta ya kunyunyuzia katika wali 3 table spoon
Zaafarani au rangi ya biriani kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1· Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.
2· Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.
3· Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.
4· Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.
5· Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.
6· Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.
7· Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.
8· Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.
Mtindi wa kutolea Biriyani:
Mtindi 1 kikombe
Pilipili mbichi 1 ndogo
Thomu chembe mbili
Nanaa kiasi
Chumvi chembe tu
Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli