MAPISHI - Biriyani Ya Kababu
VIPIMO VYA KABABU
Nyama ya kusaga 1 Kilo
Thomu na tangawizi ya kusagwa 1 kijiko cha supu
Vitunguu vilivyokatwa vidogo
vidogo (chopped) 2
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo
(chopped) 1 kikombe
Chumvi kiasi
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau (cumin powder) 1 kijiko cha chai
Gilgilani iliyosagwa (Corriander powder) 1 kijiko cha chai
Mdalisini wa unga ½ kijiko cha chai
Chenga za mikate (Bread crumbs) 1 kikombe
Mayai 2
VIPIMO VYA WALI NA MASALA
Mchele (Basmati) 5- 6 Vikombe
Vitunguu 6 vya kiasi
Mafuta ½ kikombe
Nyanya zilizokatwa ndogo (chopped) 4 kubwa
Pilipili mboga ya kijani kata
ndogo ndogo 2
Pilipili mbichi nzima 3
Garam Masala 1 Kijiko cha supu
Hiliki ya unga ½ kijiko cha chai
Mtindi (Yoghurt) ½ kikombe
Nyanya ya kopo 2 Vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Mafuta ya kunyunyzia katika wali 3 vijiko vya supu
Zaafarani au rangi za biriani
ya manjano na kijani kiasi.
NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA
KABABU
1. Changanya nyama, na vitu vyote ispokuwa mayai na chenga za mkate .
2. Tia mayai uliyoyapiga pamoja na chenga za mkate na changanya vizuri.
3. Fanya madongo ya umbo la yai (oval) kisha panga katika treya ya oveni na uchome kababu katika oven.
4. Epua zikiwa tayari na ziweke katika treya au bakuli utakalopikia biriani.
MASALA
1. Tia mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu hadi viwe vyekundu.
2. Tia nyanya, pilipili mbichi, pilipili mboga, bizari zote, chumvi na kaanga kidogo.
3. Tia nyanya ya kopo kisha tia mtindi, iache kidogo katika moto, kisha mimina juu ya kababu na uchanganye pamoja.
4. Chemsha mchele uive nusu, tazama kiini kama kawaida, kisha chuja na umimine juu ya masala.
5. Tia rangi za biriani kama ni zaafarani au rangi ya manjano na kijani juu ya wali kidogo, nyunyizia mafuta kidogo na changanya kidogo tu juu ya wali .
6. Funika kwa foil paper na pika katika oveni moto wa 450 Deg kwa muda wa dakika 20 hivi.
7. Epua na pakuwa wali katika sahani kisha masala juu yake ikiwa tayari kuliwa.
KIDOKEZO: Ni vizuri kutumia treya za oven za foil (Foil paper tray)